Imeandikwa na Mwandishi Wetu
WAKATI Rais John Magufuli na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni, leo
wanaweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa ujenzi wa bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda hadi hapa Tanga, Tanzania, maandalizi yote ya
uzinduzi wa mradi huo wa kihistoria yamekamilika, humu mji ukifurika na
kupeleka neema kwa wafanyabiashara wa nyumba za wageni, vyombo vya
usafi ri na kadhalika.
HabariLeo jana lilitembelea Chongoleani na kukuta wahusika
wakikamilisha ujenzi wa jukwaa, upangaji viti na uwekaji wa mahema. Juzi
katika eneo hilo hilo, gazeti hili pia ilishuhudia wazee wa eneo mitaa
ya Putini na Chongoleani wakiomba dua ili shughuli ya leo na
zitakazoendelea kufanyika katika eneo hilo zipate baraka za Mwenyezi
Mungu.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na Meya wa Mji wa Tanga,
Seleboss Mustafa, wamewataka wananchi wa Tanga kujitokeza kwa wingi
kushuhudia uwekaji huo wa jiwe la msingi la ujenzi wa bomba hilo
linalotazamiwa kuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa wakazi wa mkoa wa
Tanga na Tanzania kwa ujumla.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment