MBUNGE LUSHOTO AWATAKA MAAFISA UGANI KUACHA KUKAA OFISINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


MAAFISA Ugani wa Kata na Vijiji wilayani Lushoto mkoani Tanga wametakiwa kuacha tabia ya kukaa ofisini badala yake wahakikisha wanakwenda kwa wakulima ili kuwapa elimu ya namna ya kulima kilimo cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao yao. 

Kauli hiyo ilitolewa na Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM) Shabani Shekilindi alimaarufu Bosnia wakati wa ziara yake wa kuwatembelea wananchi katika vijiji mbalimbali iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kujikita kwenye shughuli za uzalishaji na kusikiliza kero zinazowakabili.
Akiwa kwenye kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola, Mbunge huyo alisema wapo baadhi ya maafisa ugani wamekuwa wakikaa ofisini badala ya kwenda wa wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo ili waweze kuwapa elimu ya namna ya kulima kisasa jambo ambalo limekuwa likichangia kurudisha maendeleo yao nyuma. 

“Ndugu zangu maafisa ugani tambueni kuwa mnajukumu kubwa la kuhakisha mnakwenda kwa wananchi kuwaelimisha juu ya kulima kilimo chenye tija kwao kwani hiyo itawasaidia kuweza kupata mafanikio kuliko wanavyofanya sasa lakini pia acheni kukaa ofisini “Alisema.
“Kwani elimu ambayo mnaweza kuitoa inaweza kuwa chachu ya wakulima kuweza kulima mazao mazuri yatakayokuwa ya ushindani na soko la kisasa hivyo jambo hilo ni muhimu sana “Alisema. 

Alisema iwapo wakulima wataweza kufikiwa kwa wakati wataweza kuongeza tija kwenye uzalishaji ili kuweza kujiandaa vema na ujio ya fursa mbalimbali za miradi mikubwa inayokuja mkoani hapa ikiwemo bomba la mafuta ghafi kutoka hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga. 

“Niwaambie ndugu zangu hii ni fursa muhimu kwa mkoa wa Tanga na wakulima ambao walikuwa wanazalisha mazao yao na kupeleka Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa laki nane hadi tisa lakini sasa mtakuwa mkitumia hata laki nne mpaka Tanga mjini kwani mradi ukianza kutakuwa na soko la uhakika”Alisema. 

Aidha pia mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima
kubadilika kwa kuongeza uzalishaji kutokana na uwepo wa soko la uhakika kwenye mazao yao katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa kwa lengo la kuinua vipato vyao. 

Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwandai Kata ya Mlola wilayani humo,Juma Khamisi alimuhaidi mbunge huyo kuwa watashirikiana na maafisa ugani waliopo kwenye maeneo yao ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya kulima kilimo chenye tija ili waweze kunufaika. 

“Mh Mbunge tumepokea kauli yako kwa mikono miwili na sisi kama viongozi wa kijiji hiki tutahakikisha tunashirikiana na maafisa ugani,wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji ambao utakuwa chachu ya kuweza kuwainua kiuchumi kwa kuchochoea kasi ya maendeleo kwao “Alisema.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

MAMIA WAMZIKA MKE WA MWANDISHI WA HABARI WA GAZETI LA MWANANCHI MKOANI TANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwa nyumbani kwa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi mkoani Tanga,Burhan Yakub ambaye alifiwa na mkewe wakati wa mazishi ambayo yamefanyika leo Makaburi ya Magomeni Jijini Tanga
Sehemu ya waombolezaji wakiwa wamelibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mke wa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga wakilipeleka makaburini tayari kwa ajili ya maziko.
 Sehemu ya waombolezaji wakiwa msibani eneo la Magomeni Jijini Tanga
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Tanga wakiwa msibani leo katikati mwenye tisheti ya mistari ni Mwandishi Mwandamizi wa ITV na Radio One mkoani Tanga,William Mngazija kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga,Hassan Hashim
 Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoani Tanga,Burhan Yakub kushoto ambaye amefiwa na mkewe akiwa na ndugu jamaa wakati wa msiba huo nyumbani kwake eneo la magomeni Jijini Tanga.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akiingia kwenye eneo la Msiba leo
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akiwa eneo la msibani Magomeni Jijini Tanga kulia ni Katibu Itikadi na Uenezi CCM wilaya ya Tanga,Lupasio Kapange

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akisalimiana na wananchi waliokuwepo msibani mara baada ya kuwasili
Wananchi wakifukia mwili wa aliyekuwa mke wa Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi mkoani Tanga,Burhan Yakub
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Tanga,Allan Kingazi wakati wa mazishi hayo
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mustapha Selebosi
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Tanga,Hassan Hashimn akiteta jambo na wandishi wa habari mkoani Tanga wakati wa msiba huo(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

SERIKALI NA UMOJA WA MATAIFA ZAUNGANA NA MRADI WA DUNIA WA XPRIZE ILI KUWAPATIA WATOTO 2,400 ZANA YA KITEKNOLOJIA YA ELIMU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Taarifa ya Pamoja kwa Vyombo vya Habari

11 Desemba, 2017

SERIKALI NA UMOJA WA MATAIFA ZAUNGANA NA MRADI WA DUNIA WA XPRIZE ILI KUWAPATIA WATOTO 2,400 ZANA YA KITEKNOLOJIA YA ELIMU

WILAYA YA MUHEZA, TANGA, TANZANIA – Katika sherehe zilizofanyika katika kijiji kimoja huko mkoani Tanga, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) yaligawa tableti zilizowekewa mfumo wa elimu kwa watoto. Tableti hizo ziligawiwa kama sehemu ya mradi wa majaribio wa miezi 15 chini ya Global Learning XPRIZE, ambao ni mradi wa miaka mitano uliotokana na mashindano duniani yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 15. Mradi huu wa dunia unatoa changamoto kwa timu za wabunifu kubuni na kuandaa zana-wazi za kiteknolojia ili kuwawezesha watoto walio na fursa ndogo ya kupata elimu katika umri wa miaka tisa hadi kumi na mmoja, kujifunza wenyewe stadi za msingi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

VIONGOZI WILAYANI HANDENI WASHIRIKI UJENZI KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI NGUVU KAZI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na viongozi wengine wakishiriki kujaza zege kwenye ndoo kwaajili ya kumwaga kwenye jamvi la matundu ya vyoo.
 Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akishiriki kujaza zege kwa ajili ya kumwaga kwenye jamvi la matundu ya vyoo na viongozi wengine.
 Mkuu wa Wilaya na Viongozi wengine wakikagua moja ya darasa Shule ya Sekondari Kiva.
 fundi mkuu wa ujenzi wa madarasa na vyoo akitoa maelezo kwa viongozi juu ya ujenzi wa matundu ya vyoo​
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea kushiriki ujenzi wa matundu ya vyoo.

DC HANDENI ATOA SIKU 14 WATAALAMU WA ARDHI KUAINISHA MPAKA UNAOTENGANISHA HALMASHAURI YA WILAYA NA MJI KATA YA MISIMA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe akizungumza na wafugaji   wa Kijiji cha Msomera na akiwasisitiza kuwa Kuwa Kijiji hicho ni cha wafugaji wote bila kujali kabila.
 Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw.William Makufwe akiwaeleza wafugaji wa Kijiji cha Msomera kuwa  wakulima kuingia kwenye eneo la kufugia mifugo kunatokana na baadhi ya viongozi kutokuwa waadilifu kwa kuuza maeneo bila kufuata taratibu na kuwataka kushirikisha wananchi kwa kila jambo kwani viongozi sio watu wenye maamuzi ya mwisho.
Baadhi ya wafugaji na wakulima walioshiriki mkutano wa hadhara.
 mmoja wa wafugaji akitoa malalamiko yake kuhusu wakulima kuvamia eneo la mifugo na kuanza kulima kinyume na taratibu na kuomba kuanishiwa mipaka kuepuka muingiliano.


Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.Godwin Gondwe amewapa siku 14 wataalamu wa ardhi wa Wilaya kuainisha mipaka baina ya Kata ya Misima iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Halmashauri ya Mji ili kuondoa mkanganyiko wa mpaka uliodumu kwa muda mrefu. 

Mkuu wa Wilaya ameyazungumza hayo jana alipokuwa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika kwenye Kijiji cha Msomera Kata ya Misima baada ya uongozi wa Kijiji hicho kuomba msaada wa kusikilizwa ili kuainishiwa mipaka baina ya Kata na Vijiji ili kuondoa muingiliano.

Mh. Gondwe alisema kuwa wataalamuwa ardhi watapima na kuonesha mipaka baina ya Halmashauri ya Mji na Wilaya ili wafahamu mipaka yao na kutambua wanapaswa kuitika wapi na kuondoa migongano inayokwamisha wananchi kushiriki katika maendeleo.

Alisema kuwa Msomera ni Kijiji kilichoanzishwa kisheria na kipo kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi hivyo wananchi wote wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria na kuwataka wananchi wote wanaokuja kwenye Kijiji hicho na maeneo mengine kufuata masharti ya maeneo husika kwani Tanazania ni huru kuishi kwa kila mwananchi isipokuwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.

MEYA WA JIJI LA TANGA APOKEA VIFAA TIBA KUTOKA KUWAIT

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem (kushoto) akimkabidhi mabeseni 50 yenye vifaa tiba kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto wachanga, Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhina Mustapha Selebosi ,kulia 
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem atia saini katika kitabu cha wageni mara alipowasili katika uzinduzi wa Kisima 
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem amezindua visima sita vya maji safi na salama katika Mkoa wa Tanga mwisho wa wiki,ikiwemo shule ya Old Tanga Secondary School vilivyochimbwa na Jumuiya ya Direct Aid ya Kuwait ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi huo.

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem amezindua visima sita vya maji safi na salama mwisho wa wiki katika Mkoa wa tanga ikiwemo shule ya Old Tanga Secondary School ,vilivyochimbwa na Jumuiya ya Direct Aid ya Kuwait ikiwa ni mwendelezo wa mradi ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait nchini unaofahamika kwa jina la “KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE”, uzinduzi ambao ulihudhuriwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhina Mustapha Selebosi, walimu, wanafunzi na wadau mbalimbali.

Aidha Balozi wa Kuwait alitembelea kituo cha afya cha Ngamiani ambapo alimkabidhi Mstahiki Meya wa Tanga mabeseni 50 yenye vifaa tiba kwa ajili ya akina mama wajawazito na watoto wachanga, mabeseni ambayo ni msaada kutoka taasisi ya Red Crescent ya Kuwait. Akiwa mjini Tanga Balozi Al-Najem alihudhuria mahafali ya kuhitimu wanafunzi wa Shule ya sekondari ya Kheri ya wanawake.

Kwa upande wake Meya wa Tanga aliushukuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa msaada huo na akamuomba Balozi wa Kuwait pia aweze kusaidia katika shule za jiji hilo 98 za msingi na 32 za sekondari Rkupata huduma ya visima vya maji.

LUSINDE AUWASHA MOTO KOROGWE MKOANI TANGA WAKATI WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde  akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM kwani ndiye ambaye anaweza kuwapa maendeleo kwa haraka zaidi
 Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde  akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde kushoto akimnadi mgombea udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduizi (CCM) Mustapha Shengwatu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba sokoni wilayani humo
 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini,Nassoro Hemedi Malingumu akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini Emanuel Charles akizungumza katika mkutano huo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hizo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi wa Kata ya Majengo kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kushirikiana naye kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi zaidi
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuhakikisha hawafanyi makosa kwa kumpa kura nyingi za kutosha mgombea udiwani wa CCM kwani dhamira yake ni kuhakikisha anawapatia maendeleo kwa kiwango kikubwa
Katibu wa CCM Korogwe Mjini Ally Issa Ally akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo katika Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustapha Shengwatu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni 


 Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi katikati akifuatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda na kushoto ni Mgombea Udiwani wa CCM Mustapha Shengwatu
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi huo katikati anayeshughudia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji akisalimiana na makada wa CCM mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni  wakati wa uzinduzi huo kampeni za mgombea Udiwani kupitia chama hicho kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji katikati akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Tanga kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kulia ni Katibu wa CCM Korogwe Mjini,Ally Issa Ally na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakiingia uwanja wa Sabasaba sokoni tayari kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa CCM Kata ya Majengo.
 Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu kushoto akifuatilia kwa umakini hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde alimaarufu Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mjini huku akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM
 Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia kampeni hizo
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa