Home » » RAIS MUSEVENI AWASILI JIJINI TANGA TAYARI KWA SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI HAPO KESHO

RAIS MUSEVENI AWASILI JIJINI TANGA TAYARI KWA SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI LA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI HAPO KESHO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (haonekani pichani) na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga akiwa ameongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kupokewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa tayari kwa Sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi toka Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania utakaofanyika  Agosti 5 2017 katika eneo la Chongoleani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri  Kaguta Museveni  mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo jijini  Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri  Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Ikulu ndogo jijini Tanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wakati kwenye Dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Ikulu ndogo jijini Tanga.  Pamoja nao meza kuu ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Mama Janeth Magufuli. 
Picha na IKULU
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa