Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongeza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akitoa neon la utangulizi wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers Dkt. Jim Yonaz akielezea kuhusu malengo ya kongamano la Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
amewataka wakazi wa na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kuanza mapema
kuzitumia fursa zilizopo katika mkoa huo kabla ya wageni hawajazitu,ia
na kuwaacha wenyeji kuwa watazamaji.
Waziri
Mwakyembe ametoa rai hiyo leo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano
la siku moja la Fursa za Biashara ambalo lina lengo la kufungua fursa za
biashara zilizopo katika mkoa na hasa katika kipindi hiki ambacho
ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani
jijini Tanga unatarajiwa kuanza.
“Tusipojipanga
leo na kuzitumia vizuri hizi fursa nyingi zilizopo basi tujue fursa
hizi zitatumiwa na wageni ili hali Watanzania tunaauwezo”, alisisitiza
Waziri Mwakyembe.
Alieleza
kuwa kama kuna changamoto zozote zinazowakabili watu wa Tanga na
Watanzania kwa ujumla katika kutumia fursa zilizopo basi ni vema
Serikali ya Mkoa, wafanyabishara na wawekezaji waliopo mkoa wa Tanga
wakazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili zigeuke kuwa fursa ili
Watanzania wazichangamikie.
0 comments:
Post a Comment