Home » » SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA MPAKA CHONGOLEANI, TANGA ZAENDELEA HIVI SASA

SHEREHE ZA UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI BOMBA LA MAFUTA GHAFI KUTOKA HOIMA MPAKA CHONGOLEANI, TANGA ZAENDELEA HIVI SASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.  

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga, katika sherehe iliyofanyika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga leo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.



Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakifurahi jambo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakiwa katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kushoto), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa wamesimama wakati wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wananchi wakishangilia wakati Rais Dkt. John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Uganda, Yoweri  Kaguta Museveni  wakiwasili katika viwanja vya Chongoleani, Mkoani Tanga tayari kwa sherehe za uwekaji wa jiwe la Msingi la ujenzi wa  mradi mkubwa wa usafirishaji wa Mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda mpaka katika bandari ya Tanga.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa