Imeandikwa na Isdory Kitunda
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi amesema
imenzisha programu maalumu ambayo itasaidia kuondoa migogoro ya ardhi
baina ya hifadhi na wananchi wanaouzunguka maeneo hayo.
Kijazi ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa
wahariri na wanahabari waandamizi wa vyombo vya habari mbalimbali nchini
unaofanyika jijini Tanga. "Programu hii ambayo tumeianzisha itasaidia
sana kuondoa migogoro na wananchi wanaozunguka hifadhi mbalimbali
zilizopo hapa nchini," amesema Kijazi.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment