Imeandikwa na Katuma Samba
Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amesema kwa
kiasi kikubwa serikali imefanikiwa kupambana na tatizo la ujangili hatua
iliyosababisha ujangili huo kupubgua kwa kiasi kikubwa.
Aidha, amevipongeza vyombo vya habari kwa kufanikisha vita hiyo huku
akivitaka kuendelea kuandika zaidi ili kuweza kumaliza vita hiyo.
Waziri Maghembe ameyasema hayo leo wakati akifungu mkutano wa mwaka
wa Wahariri na Wanahabari waandimizi wa masuala ya utalii ambao
umeandaliwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ambao unafanyika
Tanga kuanzia leo.
"Unajua vile mnavyoandika imesaidia juwaelimisha wananchi kuacha
kujishughulisha na mambo ya ujangili, tumefanikiwa kupunguza ujangili
kwa kiasi kijubwa, endeleeni kuandika kuhusu vita hii," amesema Waziri
Maghembe.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment