Na Adili Mhina, Tanga.
Timu ya ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya
Mipango ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Bibi Florence
Mwanri imefanya ziara katika Kiwanda cha Tanga Cement kilichopo Mkoani
hapa kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda
hicho.
Katika
ziara hiyo, Bibi Mwanri alipata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya
kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na eneo linalotumika kuchimba malighafi za
kutengenezea saruji, teknolojia ya kisasa inayotumika kuendesha mashine
kiwandani hapo pamoja na kuangalia hatua mbalimbali zinazotumika katika
uzalishaji wa saruji.
Akiwa
katika eneo linalochimbwa mawe ya kutengenezea saruji, Mwanri alieleza
kuwa kiwanda hicho kina wajibu wa kuhakikisha sheria na
taratibu za utunzaji wa mazingira zinazingatiwa muda wote ili
kuhakikisha mazingira yanabaki salama licha ya shughuli za uchimbaji
kuendelea kufanyika.
Mwanri
alipongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuendelea kutekeleza majukumu
yake katika kuunga mkono dhamira ya Serikali ya kuwa nchi ya Viwanda na
kuharakisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo inayosisitiza kufikia
uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Naye Meneja wa Kiwanda hicho, Mhandisi Ben Lema alisema kuwa kiwanda hicho kimeendelea kutoa
ajira kwa watanzania katika kada mbalimbali ambapo kwa sasa kua ajira
zaidi ya 600 ambapo ajira 300 ni za moja kwa moja huku ajiara 300
zingine ambazo sio za moja kwa moja zinajumuisha wauzaji, wasambazaji,
wasafirishaji na wengine walioko katika mnyororo huo.
Aliongeza kuwa bidhaa za kiwanda hicho bado zinafanya vizuri sokoni licha ya ushindani uliopo kufuatia kuanzishwa kwa viwanda vingi vinavyozalisha saruji kwa kuwa mahitaji ya saruji bado ni mwakubwa sokoni.
Lema
alieleza kuwa viwanda vya saruji vinapata faraja kubwa kwa kuwa miradi
mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na Serikali na hata inayotekelezwa
na sekta binafsi inatumia saruji inayotengenezwa na viwanda vya ndani.
0 comments:
Post a Comment