Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
Serikali
kupiti Bunge lake Tukufu limetoa pongezi kwa kampuni ya Azam Marine kwa
kuanza kutoa huduma za usafiri kati ya Mkoa wa Tanga na Pemba.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani
alizitoa pongezi hizo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali
la Mbunge wa Tanga Mjini juu ya mpango wa Serikali wa kununua meli ya
kisasa na ya uhakika ili kuokoa wasafiri wa Tanga na Pemba.
“Tarehe
29 Januari, 2017 kampuni ya Azam Marine imeanza kutoa huduma ya usafiri
wa abiria na mizigo kati ya Pemba na Tanga kwa kutumia Meli ya Sealink 2
yenye uwezo wa kubeba abiria 1,650 na mizigo tani 717,” alifafanua
Mhandisi Ngonyani.
Aliendelea
kwa kusema kuwa Januari 31, 2017 Meli ya Sealink 2 iliondoka Tanga saa
3:00 asubuhi kwenda Pemba hadi Unguja. Aidha Meli hiyo itafanya safari
zake mara moja kwa wiki baina ya Pemba na Tanga hadi pale ambapo idadi
ya mizigo itakapolazimu kuongeza safari nyingine.
Mhandisi
Ngonyani amesema kuwa Serikali inaipongeza kampuni hiyo kwa kuitikia
wito wa kuanzisha huduma ya usafiri majini baina ya Tanga, Unguja na
Pemba hivyo kuondokana na changamoto za usafiri zilizokuwa zikiikabiri
mikoa hiyo.
Aidha
ametoa wito kwa wawekezaji wengine kupeleka vyombo vya usafiri vya
kisasa majini ili kuongeza huduma ya usafiri katika maeneo
yanayokabiliwa na changamoto ya usafiri kupitia njia ya majini.
Vile
vile amewataka wananchi wanaosafiri kati ya Pemba na Tanga kutumia
huduma za meli salama na kuachana na vyombo visivyo salama vinavyo
hatarisha maisha na mali zao.
Mwisho…
0 comments:
Post a Comment