Tanga, WAJUMBE 14 wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi Baraza la Uwakilishi la Zanzibar wamesema ujio wa Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga litaongeza ajira kwa vijana wakiwemo Wanzanzibar waishio Tanga.
Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea bandari ya Tanga eneo la upakuzi wa shehena ya mizigo na eneo itakapojengwa bandari mpya ya Mwambani.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Hassan
alisema Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari zake ikiwemo
ya Wete na Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Bomba
la Mafuta.
Akizungumzia kilio
cha wafanyabiashara na wasafiri wa Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri
wa baharini, Hassan alisema kero hiyo Serikali inaitambua na jitihada za
kuwa na meli ya uhakika inafanywa.
Alisema
kuna baadhi ya wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa wakichukua
bidhaa Tanga wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na
kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika wa baharini.
Awali
akizungumza na wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi, Kaimu Meneja wa
Badari Tanga, Henry Arika, alisema mchakato wa mradi wa bomba la mafuta
unaenda kwa kasi na kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja kuwekeza.
Alisema Tanga ziko fursa nyingi za uwekezaji na yako maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa mradi wa Bomba la mafuta amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe 14 wa Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar walipotembelea bandari ya Tanga kujifunza
Afisa Mtekelezaji Mkuu Bandari ya Tanga, Donald Kaire, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar walipofanya ziara bandari hiyo juzi. Katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika.
0 comments:
Post a Comment