Home » » TRA YAKUSANYA SHILINGI TRILIONI 1.15 MWEZI OKTOBA.

TRA YAKUSANYA SHILINGI TRILIONI 1.15 MWEZI OKTOBA.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Ally Daud-MAELEZO
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikia kukusanya shilingi trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba ikiwa ni kukamilisha malengo waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi Bw. Richard Kayombo wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu  hali ya makusanyo na zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi (TIN)linaloendelea hivi sasa.
“Tumefanikiwa kukusanya shilingi Trilioni 1.15 kwa mwezi Oktoba mwaka huu ikiwa ni kufanikisha malengo ya ukusanyaji kodi nchini ili kukuza uchumi wa nchi pamoja kusaidia Serikali kuendeleza huduma za jamii nchini” alisema Bw. Kayombo.
Aidha Bw. Kayombo amesema kuwa mapato hayo yametokana na mikakati thabiti iliyowekwa na mamlaka hiyo katika ukusanyaji kodi hapa nchini ili kuweza kusaidia ongezeko la pato la Taifa .
Katika hatua nyingine TRA imefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 zilizokuwa zikiendelea katika mahakama mbalimbali nchini dhidi ya walipa kodi wake na kufanikiwa kupata kiasi cha takribani Bilioni 16.9 .
“Tumefanikiwa kushinda kesi 9 kati ya 10 ambazo zilifikishwa mahakamani dhidi ya walipa kodi na kupata kiasi cha shilingi bilioni 16.9 hivyo kufanya juhudi zetu za kukusanya mapato mengi zaidi” aliongeza Bw. Kayombo.
Mbali na hayo Bw. Kayombo amesema kuwa zoezi la uhakiki wa namba za utambulisho wa mlipa kodi ambalo limeanza hivi karibuni linaendelea na litafikia tamati Novemba 30 mwaka huu kwa mkoa Dar es salaam hivyo wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya uhakiki huo.
Aidha Bw. Kayombo ameongeza kuwa  kila mwenye namba ya utambulisho wa mlipa kodi anatakiwa akahakiki kwa ajili ya kupata taarifa sahihi za mlipa kodi ili kuepuka kufutwa kwa  namba yake ya utambulisho baada ya zoezi hilo kumalizika kwa mkoa husika.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa