Na Anitha Jonas – MAELEZO, Tanga
Tanga.
Serikali imeagiza Maafisa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mikoani kuanza kushirikishwa katika vikao vya maamuzi ili wapate
kujua mikakati ya maendeleo kwa sekta zao.
Agizo hilo limetolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Annastazia Wambura alipokuwa katika ziara ya
kikazi Jijini Tanga kwa ambapo lengo la
ziara hiyo ilikuwa ni kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kisekta kwa Wizara
yake katika Mkoa huo.
Mheshiwa Naibu Waziri Wambura alisema kushirikishwa katika
vikao vya maamuzi kwa watendaji wa Kada hizo kutasaidia kuongeza chachu ya ukua
wa sekta hizo katika mikoa pamoja na kutoa maoni ya kitaalum kwa sekta hizo
kutoka kwao.
“Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 mtenge bajeti ya Kitengo cha Habari
na pia mfanye utaratibu wa kupata Maafisa Habari kwa kuanzia ngazi ya
Mkoa,Wilaya ,Halmashauri,pamoja na Jiji kwani kada hii ni muhimu kuwepo kwa lengo lakusaidia kutangaza
maendeleo na fursa zilizopo katika Mkoa wenu”,alisema Mhe .Wambura.
Pamoja na hayo Mhe. Naibu Waziri Wambura aliendelea kusema
Serikali inataka wananchi wapate kujua shughuli zote za maendeleo katika Mkoa
wao zinafanyika vipi na mikakati ya maendeleo iko vipo,hivyo ni muhimu kupata
Maafisa Habari watakao wasaidia kufanikisha hilo kazi ya kutoa habari hizo kwa
umma.
Aidha, Naibu Waziri huyo alisisitiza kuwa Wizara kwa sasa ipo
katika mazungumzo na TAMISEMI kwa jili ya kubadili mfumo na kuanzisha Kurugenzi za kisekta kwa Maafisa
Habari,Maafisa Utamaduni,Maafisa Sanaa na Maafisa Michezo katika ngazi za Mikoa lengo ikiwa ni
kuimarisha sekta hizo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martin Shigela
alisema Mkoa huo unakabiliwa pia na uhaba wa Maafisa Michezo ,Maafisa Utamaduni
na Maafisa Sanaa katika Mkoa na Halmashauri lakini suala hilo tayari
wameanza kulifanyia kazi kwa kufanya utaratibu wa kupata Maafisa hao.
Halikadhalika naye
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mjini Bw. Thobias Mwilapwa alimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa ziara
yake kwa kuwa ametoa somo zuri la
utendaji na pia anaamini atafanyia kazi kilio cha wadau wa michezo wa mkoa huo
kwani ni mmoja wapo katika historia ya
Michezo ,pamoja na Muziki wa Mwambao
(Taarabu) pamoja na Mchezo wa Mbio za Baiskeli.
Pamoja na hayo naibu waziri huyo alitoa wito kwa wakazi wa
Tanga katika kipindi wanapokuwa wakifanya shughuli za kimila na desturi kama za Jando na Unyago basi wawashirikishe
wataalam wa Afya pamoja na wa Elimu kwa lengo la kutoa elimu ya afya ya uzazi
halikadhalika kuelezewa umuhimu wa elimu katika maisha ya vijana wanaofanyiwa
shughuli hizo.
Hata hivyo wakazi wote
wa mkoa wa Tanga wametakiwa kuongeza
juhudi za kusimamia muenendo mzuri wa maadili ya kitanzania ikiwa ni jukumu la
kila mtu pamoja na kufanya kazi kwa kujituma zaidi kama kauli mbiu ya
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya HAPAKAZI TU!
0 comments:
Post a Comment