Anitha Jonas –
MAELEZO
Tanga
Serikali imepongeza
taasisi isiyo ya Kiserikali ya Makumbusho
Urithi Tanga kwa jitihada nzuri walizofanya za kuandaa
makumbusho itakayo hifadhi utamaduni wa wakazi wa Mkoa wa Tanga.
Pongezi hizo
zimetolewa leo jijini Tanga na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo alipotembelea Makumbusho hayo ya Urithi Tanga alipokuwa katika ziara
yake ya kikazi mkoani hapo iliyolenga
kujua uendeshwaji wa shughuli za kisekta.
“Kazi hii ya
ukusanyaji wa taarifa mbalimbali za wakazi wa Tanga kuanzia ngazi ya Makabila
yote saba ya Mkoa wa Tanga,Mila na Desturi
zao, pamoja na kuhimiza ukarabati majengo ya kale kweli mnahitaji pongezi kwa
uzalendo huo”,
“Serikali ya China
iliahidi kusaidia kujenga Majumba ya Makumbusho kwa nchi za Afrika hivyo andikeni
barua ya Wizarani kuwa ajili ya kuendeleza makumbusho haya halafu
tutaiwasilisha Ubalozi wa China”.alisema Naibu Waziri Wambura,
Kwa upande Mkurugenzi
wa Makumbusho ya Urithi Tanga Mhandisi Godwin Mhando alisema lengo la
kuanzisha makumbusho hayo ilikuwa ni kutaka kutunza historia ya Mkoa wa Tanga
pamoja na kulinda kuhifadhi Mila na Desturi za watu wa Tanga kwa ajili ya
vizazi vijavyo kwani Mkoa huo unahistoria
kubwa katika nchi.
“Makumbusho haya ya
Urithi Tanga siyo kwa maslahi binafsi bali kwa wanatanga wote na tumeamua
kufanya uhifadhi huu kwa kuwa tumeona ipo haja ya kuhifadhi historia Mkoa
wetu.”alisema Mhandisi Mhando.
Naye Mkuu wa Wilaya
ya Tanga Thobias Mwilapwa alisema ofisi
yake itajitahidi kushirikiana na viongozi wa makumbusho hayo kwa kuhakikisha
inafikia malengo iliyojiwekea kwa maslahi ya wakazi wa Tanga pamoja na Watanzania
wote kwa ujumla.
Aidha Mkurugenzi huyo
wa makumbusho aliendelea kusema kupitia ofisi hiyo wamekuwa wakipanga siku
ambayo hufanya maonesho ya shughuli za kiutamaduni kama matibabu ya
kiasili,kuwepo kwa vyakula vya asili hii ikiwa ni siku ya maadhimisho ya kuenzi utamaduni wa wakazi wa Tanga.
Hata hivyo kila Mtanzania ametakiwa kujali asili yake pamoja utamaduni
wake na pia kuenzi kwani ni urithi mkubwa kwa vizazi vijavyo.
0 comments:
Post a Comment