Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) jana limefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka
katika Ukumbi wa Hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo mgeni Rasmi
alikua ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza.
Katika
hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Mahiza aliushukuru uongozi wa
TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa ambao pia
ulifanyikia katika mkoa wake wa Tanga.
Akiongea
na wajumbe wa mkutano mkuu, Mahiza alisema, TFF ina changamoto ambazo
inapaswa kuzifanyia kazi kwa na hasa katika kuendeleza soka la wanawake
nchini ambalo bado mwamko wake uko chini sana.
Mahiza
alisema, Mpira wa miguu kwa sasa ni ajira nzuri ambayo inasaidia
kujikwamua kiuchumi kwa wachezaji pamoja na familia zao, nayaomba
makamouni yajitokeze kuwekeza katika mpira wa miguu na hasa katika soka
la wanawake.
“Mahitaji
ya wanawake katika kushiriki/kucheza mpira wa miguu ni makubwa zaidi,
tofauti na wanaume hivyo kuangalia jinsi gani wadhamini wanapatikana ili
kuweza kuwasaidia wanawake” alisema Mahiza.
Mkutano
ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni Uhakiki wa
Wajumbe, Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita, Yatokanayo na
Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, Taarifa kutoka kwa
Wanachama, Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
Zingine
ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013, Kuthibitisha ripoti
ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya 2015, Marekebisho ya
Katiba, Mengineyo na Kufunga Mkutano.
Baada
ya majadiliano ya kina mkutano mkuu pia uliazimia kuahirisha ajenda ya
marekebisho ya Katiba hadi Mkutano Mkuu ujao utakaofanyika mwezi Disemba
mwaka huuu.
Wakati
huo huo Leo Jumapili asubuhi Mkuu wa Mkoa Tanga, Mwantumu Mahiza
ameweka jiwe la msingi katika eneo la kituo cha michezo cha kukuzia
vipaji lilipo eneo la Mikanjuni jijini Tanga.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi, Mahiza alisema
wamejisikia faraja mkoa wa Tanga kupata nafasi hiyo kuwa mkoa wa kwanza
kupata kituo cha kukuzia vipaji nchini.
Mahiza
alisema uongozi wa Serikali mkoa wa Tanga utashirikiana na Chama cha
Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)/TFF katika kusaidia usimamizi wa
uendeshaji wa kituo hicho.
Mahiza
ameishukuru TFF kwa kuamua kuwekeza katika ujezi wa kituo hicho, ambacho
baaade kitatoa nafasi kwa vijana kupata ajira kupitia mpira na shughuli
nyingine za maendeleo ya kiuchumi ikiwemo utalii na watu kupata ajira
katika kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment