Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Mihayo Msikhela
MGANGA wa tiba za asili, Juma Ramadhani pamoja na mwanafunzi wa Chuo
cha Utalii Masai, Saumu Mohamed (19) wanashikiliwa na Polisi mkoani
Tanga kwa tuhuma za kuharibu mimba ya miezi saba.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Mihayo Msikhela aliwaambia waandishi
wa habari jana, watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa mtaa wa Sahare,
walikamatwa Februari 29 mwaka huu saa 2:00 usiku katika mtaa huo ulio
kata ya Mzingani.
Alisema kukamatwa kwao kumekuja baada ya wananchi kuokota maiti ya
mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike ambaye inadaiwa alikuwa ni mimba ya
miezi saba.
“Siku hiyo ya tukio katika maeneo ya Sahare jijini Tanga aliokotwa
mtoto wa kike ambaye ni mimba ya miezi saba. Inadaiwa mimba hiyo
iliharibiwa na Saumu ambaye in mwanafunzi wa Chuo cha Utalii Masai cha
mkoani hapa”.
Alisema na kuongeza: “Binti huyo kulingana na uchunguzi wetu wa awali
anadaiwa kunywa dawa ya kutoa mimba kwa kutumia dawa maalumu ambayo
alipewa na mganga wa kienyeji aitwaye Juma Ramadhani na ndipo ikaharibu
ujauzito huo na kisha Saumu alipofanikiwa kujifungua, akaamua kutupa
maiti ya mtoto huyo ambayo baadaye iliokotwa na wananchi.”
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa na Polisi na watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Chanzo Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment