Home » » MBUNGE WA BUMBULI MH.JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA JIMBO LAKE NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

MBUNGE WA BUMBULI MH.JANUARY MAKAMBA ATEMBELEA JIMBO LAKE NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akisalimiana na na kuwashukuru Wananchi wa Kijiji cha Mpunda pamoja na kijiji cha Kihitu vilivyopo Kata ya Vuga kwa kumchagua kuwa Mbunge wao kwa mara nyingine tena na pia kwa kumchagua Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano kupitia chama cha Mapinduzi (CCM).

Mh Makamba pia alifanya ziara a ya kukagua miradi mbalimbali  ya kimaendeleo ikiwemo sambamba na kupokea kero za Wananchi hao na kuzitafutia ufumbuzi,pia amewahidi wananchi hao kuwaletea zaidi Maendeleo katika jimbo hilo.(Picha na Imani Nsamila) .
Wananchi wa Kijiji cha Mpunda Kata ya Usambara wakimuonesha Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba eneo ambalo Wakazi hao wamepewa na Kiwanda cha Katani ili wajenge Zahanati ya Kijiji.

Katibu wa Wilaya ya Lushoto Ramadhani Mahanyo akizungumza katika Mkutano huo. 
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mpunda baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mpunda baada ya kumalizika kwa Mkutano huo,ambapo pia aliwashukuru Wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wao kwa kura nyingi,ane amewahidi kuwaletea maendeleo katika jimbo hilo la Bumbuli.
 
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba akibadilishana namba za Simu na wananchi wa Jimbo lake ili kurahisisha Mawasiliano kati yake na wanakijiji hao, wakati alipofika katika Kijiji hicho kuangalia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili kwa sasa.
(Picha na Imani Nsamila) .
 Baadhi ya Wazee wakifurahia jambo na Mbunge huyo,Mh.January Makamba

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa