Chama Cha Wananchi (CUF)
Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF, Amina Mwindau,
anayepinga ushindi wa Jumaa Awesso, inasikilizwa na Jaji Patricia
Fikirini, ambaye alisema jana kwamba atasikiliza mfululizo.
Katika shauri hilo, Amina anatetewa na Wakili Mashaka Ngole wakati
Awesso anatetewa na Kanyama Anthony na Warehema Singano. Jopo la
mawakili wa serikali wanaomtetea Mwanasheria Mkuu wa Serikali msimamizi
wa uchaguzi, linaongozwa na Martenus Marandu na Saraji Iboru.
Akitoa ushahidi huku akihojiwa na mawakili wa pande zote, Katibu wa
CUF Wilaya ya Pangani, Ramadhan Hamad, alidai kuwa alipelekewa taarifa
ofisini kwake kwamba katika mikutano ya kampeni ya CCM iliyofanyika
Madanga, Mkaramo, Mwera na Mikinguni, waliopanda majukwaani walisikika
wakitoa maeneo ya kumdhalilisha na ya ubaguzi dhidi ya Amina Mwindau.
Alidai kuwa viongozi wa CCM waliopanda kwenye majukwaa walisikika
wakisema: “Amina Mwindau katiwa mimba na Anko Moo, Amina kwao ni
Mwarongo si Pangani, Amina ni mwanamke hawezi kuongoza na uchaguzi
ukimalizika atakwenda Zambia kumfuata mumewe.”
Shahidi mwingine, Swaib Mwanyika (24) anayeishi kata ya Madanga,
aliwataja viongozi aliowaona wakipanda jukwaani Madanga kuwa ni Salim
Bahorera na Hamis Mnegero ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Pangani
kwamba walisikika wakisema ''Amina kwao Mwarongo…Amina ni Bi Kidude.''
Shahidi huyo alitoa maeneo hayo kwa kuongozwa na wakili wa Mwindau,
Mashaka Ngole lakini Jaji alilazimika kuahirisha kesi hiyo baada ya
kumhoji wakili wa Awesso, Kanyama ambaye alidai ana maswali 52 ya
kumhoji Mwanyika na kutokana na kuwa zilibaki dakika 41 kutimia saa
10.00 jioni, hawezi kufanya hivyo.
Idadi ya mashahidi waliopangwa kutoa ushahidi wao katika shauri
hilo ni 94. Mashahidi wa Mwindau ni 48 na waliobaki ni wa upande wa
Awesso.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment