KIONGOZI wa Chama cha (ACT) Wazalendo, Zitto Kabwe amesema ameibua hoja nzito na kushangazwa na hatua ya Serikali kuwapa kazi ya ujenzi wa Bandari ya Mwambani mkoani Tanga watu waliokuwa wakituhumiwa katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha (ACT) Wazalendo, kimemtaka Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, afanye uchunguzi kuhusu mradi huo wa Mwambani na achukue hatua kwa kile alichodai kuwa utapeli wa watu wa Escrow.
Alisema pamoja na kupewa kazi hiyo kupitia mradi wa Mwambani Economic Corridor Project (MWAPORC), ambao utagharimu Sh trilioni 54 huku kukiwa hakuna taratibu za utangazaji zabuni zilizofutwa na Serikali.
Zitto alitoa kauli hiyo katika mikutano wa hadhara uliofanyika miji ya Mafinga na Iringa mjini katika Uwanja wa Mwetogwa mjini.
Kiongozi huyo wa (ACT) Wazalendo alisema hatua ya Serikali ya kuwapa kazi ya ujenzi Mwenyekiti wa Kampuni ya VIP Engineering and Management, James Rugemalira.
Mwambani Economic Corridor Project. Hapakuwa na zabuni yeyote iliyotangazwa na huu Mradi umekuwa ukiandaliwa na Serikali. Sheria ya Private Public Partnership ( PPP) imeweka utaratibu wa zabuni kwa miradi ya ubia na Serikali.
Taratibu hazijafuatwa, hakuna zabuni iliyotangazwa kuhusu Mwambani miradi mikubwa kama hii Serikali hutakiwa kutoa Guarantee kwa mikopo ambayo inachukuliwa. Hivyo kuhusika kwa Rugemalira wa Escrow na mwanasheria Cathbert Tenga wa Richmond kwenye mradi huu ni muendelezo wa miradi ya kitapeli, alisema Zitto.
Zitto, ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema uzito wa mradi huo wa bandari ambao unakwenda na reli ambayo itafika hadi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Waziri Sitta na atoe taarifa kwa umma kwa Taifa limechoka na miradi aliyodai ya kitapeli.
Mwigamba na umaskini
Naye Katibu Mkuu wa (ACT) Wazalendo, Samson Mwigamba, alisema kuwa hali ya umaskini nchini imezidi kuongezeka huku viongozi wakiendelea kuponda maisha.
Wakati Rais Jakaya Kikwete, anaingia madarakani mwaka 2005 hali ilikuwa mbaya lakini bado watu walikuwa na matumaini ya kurekebishiwa hali zao, leo anakaribia kumaliza kipindi cjake cha uongozi uchumi bado unamilikiwa na watu wachache.
"Tanzania ni nchi pekee inayochimba madini ya Tanzanite, mazao yao Mirerani ni madini lakini bado Serikali ilichukua ule mgodi na kuwapa makaburu kutoka Afrika Kusini huku Watanzania wakibaki wazamaji. Pia walikuwa wakichimba huku wakiweka maji yenye sumu huku Watanzania wakiendelea kufa kwa Ukimwi na njaa, alisema
Katibu Mkuu huyo wa (ACT) Wazalendo, alisema pamoja na madini hayo kuchimbwa nchini lakini nchi ya Afrika Kusini imekuwa ya kwanza katika soko la dunia kwa kuuza madini ya Tanzanite ikifuatiwa na Kenya huku Tanzania ikishika nafasi ya tisa.
Mwigamba aliongeza ujio wa chama kipya cha (ACT)Wazalendo ni ukombozi kwa Watanzania hivyo wanachotakiwa ni kukiunga mkono kwa kuhakikisha wanapigania misngi ya kizalendo iliayoanishwa katika azimio la Arusha ambalo liliweka miiko na maadili ya uongozi.
0 comments:
Post a Comment