Taarifa zilizotufikia muda huu ambazo Hazijathibitishwa Rasmi zinasema kwamba Basi la Dar Express lenye namba za usajili T 244 BXQ limekamatwa na Gunia zaidi ya 16 za Mirungi katika kituo cha ukaguzi cha Chekeri Korogwe Likitokea Arusha Basi Hilo lilikamatwa Jana Majira ya Saa nane Mchana na kupelekwa mpaka katika kituo cha wilaya cha Polisi Korogwe, mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kuhisiwa anahusika na tukio hilo pia Konda wa Basi hilo anashikiriwa na Polisi. Endelea kufuatilia hapa Taarifa kamili inakuja mapema leo.
Basi la Dar Express likiwa limesimamishwa kwa ajili ya Ukaguzi huoUkaguzi wa Basi hilo ukiwa unaendelea
Askari wa Jeshi la Polisi wakiwa wanapakia Magunia ya Mirungi katika Gari lao
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment