KANISA la Anglikana Dayosisi ya Tanga, limeanzisha mfuko wa malipo
ya uzeeni (pensheni), kwa watumishi wake yatakayowasidia baada ya
kustaafu.
Hayo yalisemwa na Askofu wa Kanisa hilo, Mahimbo Mndolwa alipozungumza
na Tanzania Daima wakati wa hafla ya kumuaga Mchungaji wa Kigango cha
Mashewa, Thomas Ngereza iliyofanyika katika Kanisa Mtakatifu Andrews
Manundu wilayani Korogwe mwishoni mwa wiki.
Askofu Mndolwa alisema kuanzishwa kwa mafao hayo kutamsaidia mhusika
wakati atakapostaafu ili aepukane na maisha magumu yatakayowafanya
wageuke ombaomba.
“Leo tukiongozwa na Mwenyekiti wetu Dominic Singano tumemzawadia
mstaafu mabati 59; mbao, misumali kilo 10 na kumkabidhi cheti,” alisema
Mndolwa.
Alitaja baadhi ya mafao atakayopatiwa mstaafu kuwa ni nyumba, gari na
fedha ambayo anaamini yatamsaidia mstaafu huyo katika kupambana na
changamoto za maisha.
Licha ya kumuaga mchungaji Ngereza pia walikuwepo watumishi wengine
wanne waliostaafu kutoka Taasisi ya Afya na Sayansi Shirikishi ya
Mtakatifu Agustino wilayani Muheza ambao ni Mery Dismasi, Charles Juma,
Peter Rajabu na Itikija Mbaga.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment