HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imeombwa kuangalia uwezekano wa kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia manunuzi ya vifaa visaidizi kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama kwa Watu wenye Ulemavu mkoani Tanga (Shivyawata), Zuhura Mussa alipozungumza katika mahojiano na gazeti hili kuhusu changamoto zinazowakabili walemavu mkoani humo.
Vifaa hivyo vinajumuisha fimbo nyeupe na mashine za kuchapia.
Alisema kundi la walemavu linalojumuisha viziwi, wasioona, walemavu wa viungo na albino limekuwa likikumbana na changamoto hiyo kutokana na ukweli kwamba vifaa hivyo vinauzwa kwa bei ghali ambazo familia nyingi zenye walemavu hao zinashindwa kumudu gharama za kuvipata kwa urahisi.
“Tunakabiliwa na changamoto nyingi sisi watu wenye ulemavu, lakini hii ya vifaa kwetu ni kubwa hivyo tunaiomba halmashauri kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo mkoani hapa kutusaidia kupata vifaa visaidizi hivi,â€alisema Zuhura.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment