CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa kimewaagiza viongozi wa wilaya
wa chama hicho, kuwachukulia hatua kali madiwani wasiofanya ziara na
mikutano ya hadhara kwenye kata zao.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Mussa Shekimweri, alipofungua semina kwa madiwani mkoani hapa, inayofanyika katika ukumbi wa Chichi, hapa.
Shekimweri alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya madiwani licha ya kushinda katika uchaguzi, lakini hawajawahi kurudi kwa wananchi hata kutoa shukrani, jambo linaloweza kuitia doa CCM.
Azma ya kufanya hivyo ni chama kutaka kulinda heshima na kujenga mazingira ya kuendelea kukubalika kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010.
Aliwataka viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya kata kuhakikisha madiwani wanafanya ziara na mikutano ya mara kwa mara kwa wananchi. Watakaokaidi taarifa zao ziwasilishwe katika ngazi husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.
Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo amepiga marufuku madiwani kujihusisha na ukusanyaji wa michango kutoka kwa wananchi na kuwataka wawajibike katika majukumu yao.
Kazi ya diwani ni kusimamia mipango ya maendeleo na kuwasilisha kero zinazowakabili wananchi wake katika vikao vya Baraza la Madiwani na si kuchangisha michango ya kata
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment