Home » » WAGANGA WAASWA KUACHA FIKRA POTOFU

WAGANGA WAASWA KUACHA FIKRA POTOFU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini hapa, Mganga wa Asili, Mwanahawa Hasani, alisema tabia hiyo ipo kwa baadhi yao hivyo anawashauri wenye tabia ya kuagiza viungo vya binadamu waachane nayo.
“Tupo kwa ajili ya jamii na si kuipotosha, tuache jamani tabia ya kuagiza viungo vya binadamu wenzetu… hebu tuwe na roho ya huruma, uwepo wetu ni kuisaidia jamii na si kuchochea uvunjifu wa amani,” alisema Mwanahawa.
Mwanahawa, aliongeza kuna baadhi ya waganga wanaopita majumbani kwa madai ya kufichua wachawi na kuchukua tunguli za wenzao na kuondoka nazo, hivyo kuwaharibia majina jambo ambalo si jema na kuwashauri wafanye kazi kisheria na kufuata taratibu za tiba asilia zinavyowaongoza.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao, waliitaka serikali kuhakikisha waganga wote wa tiba asilia wawe na vibali na hatua zichukuliwe kwa watakaokiuka.
“Ni vyema sasa serikali ikakagua waganga wote wasiokuwa na kibali ili wawachukulie sheria, kwani wengi wao ndio wamekuwa chanzo cha kufanya kazi zao kinyume na taratibu zinavyowaongoza,” alisema Faiza Juma.
Chanzo:tanzania daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa