Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Maradhi hayo yanatokana na idadi kubwa ya
wakazi wa wilaya hiyo kukosa vyoo hivyo kujisaidia vichakani.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Muhingo Rweyemamu alipozungumza na
wakazi wa Mazingara, viongozi wa serikali ngazi ya wilaya na mashirika ya kirai kwenye ufungaji wa mradi wa World Vision Tanzania wilayani humo.
Alisema wakazi wengi wa Handeni hawana vyoo, wanajisaidia vichakani hali inayosababisha uchafuzi wa mazingira na magonjwa ya milipuko kwenye vyanzo vya maji.
“Kusema kweli hili ni tatizo kubwa… elimu inahitajika lakini maofisa afya nao wafanye kazi yao kwa mujibu wa sheria ndogo ndogo za halmashauri na kuwachukulia hatua wasio na vyoo… kikianza kipindupindu hapa ni maafa,” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Akielezea kero ya maji ilivyopunguzwa katika maeneo yenye uhaba zaidi, Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Mashariki,
Sylivester Masanja alisema Mazingara wamefanikiwa kuongeza huduma hiyo kutoka asilimia 28.5 hadi asilimia 38.5
huku baadhi ya shule, zahanati na wakazi wa vijiji wanavuna maji ya mvua.
Alisema hatua hiyo imepunguza tatizo la maji kutoka asilimia 36 hadi 62 kwa wakazi wa eneo hilo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment