Home » » SOKO LA MAHINDI NCHINI LAPOROMOKA

SOKO LA MAHINDI NCHINI LAPOROMOKA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.


SOKO la mahindi nchini limeshuka kwa mwaka huu ikilinganishwa na miaka miwili iliopita kutokana na mavuno kuwa mengi.

Wakizungumza na gazeti hili madalali wa mahindi Mkoa wa Tanga walisema soko la mahindi limeporomoka kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwa mwaka huu na kusababisha mavuno kuwa makubwa na pia kusababisha baadhi ya mahindi kuoza kipindi cha mavuno.

"Mahindi kwa mwaka huu yamekuwa mengi tofauti na miaka mingine kwani mvua zilizonyesha mwaka huu zimepelekea kustawi na kutoa mavuno ya uhakika hali itakayopelekea kupungua kwa uhaba wa chakula," alisema Mbwana Mohamedy.

Aidha baadhi ya wanunuzi wa mahindi mkoani humo walielezea hali tete ya soko la mahindi kwa mwaka inayosababisha mtandao mdogo wa uuzaji wa mahindi hali inayosababisha kuumia kwa mkulima anaeyeuza mazao yake.

Hata hivyo madalali walitoa wito kwa wakulima kuwa mwaka ujao wajitahidi kupanda mbegu zenye uwezo wa kustahmili joto pamoja na mbegu zenye uwezo wa kukaa muda mrefu ili kuepusha changamoto wanazoweza kukabiliana nazo

Chanzo;Majira

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa