Home » » RAIA WA NIGERIA WAKUTWA NA MILIPUKO TANGA

RAIA WA NIGERIA WAKUTWA NA MILIPUKO TANGA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

JESHI la Polisi mkoani hapa linawashikilia watu watatu wakiwemo raia wawili wa Nigeria kwa kosa la kukutwa na milipuko nane waliyokuwa wameihifadhi nyumbani kwa mwenyeji wao aliyejulikana kwa jina moja la Frank, mkazi wa Magoma, Korogwe.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisher Kashai, alisema Frank alikimbia mara baada ya wageni wake Kenneth Okenee (31), na Amek Boniphace (31), kukamatwa na polisi.
Kamanda Kashai, alisema tukio la kukamatwa kwa raia wa kigeni lilitokea katika Kijiji cha Kigwashi wilayani Korogwe.
Wakati huo huo, jeshi hilo linamshikilia Michael Charles (28), mkazi wa Morogoro aliyekuwa akitokea Monduli mkoani Arusha akiwa amepanda basi la abiria lenye namba T.510 aina ya Nissan Caravan akiwa na risasi 39.


Watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili,huku jeshi la polisi likitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa