Home » » MKINGA WAPEWA SARUJI MIFUKO 1,000

MKINGA WAPEWA SARUJI MIFUKO 1,000

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

KAMPUNI ya saruji Tanga imekabidhi mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara za sayansi shule za Sekondari wilayani Mkinga mkoani hapa.
Msaada huo wenye thamani ya zaidi ya sh milioni 12, utasaidia kukamilisha vyumba 38 za maabara vinavyoendelea kujengwa wilayani humo.
Akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mboni Mgaza, alisema utasaidia mapambano ya ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya wanafunzi wanaochukua masomo ya sayansi.
”Tumeshafikia mahala pazuri, imani yetu ni kwamba msaada huu wa saruji utasaidia kufikia malengo yetu tunayokusudia,” alisema Mgaza.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Rainhardt Swart, alisema saruji waliotoa ni sehemu ya mchango wa kiwanda hicho kusaidia kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Amina Kiwanika, alisema halmashauri hiyo ina shule za Sekondari 15 ambazo zina uhitaji wa vyumba 38 vya maabara kwa ajili ya wanafunzi 5,342 wanaosoma kwenye shule hizo.
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa