Home » » BIL 18/- KUTUMIKA KWA CHANJO

BIL 18/- KUTUMIKA KWA CHANJO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Bil 18/- kutumika kwa chanjo
Serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 18 kwa ajili ya chanjo ya surua na ribela inayotarajiwa kutolewa Oktoba 18 mwaka huu nchini kote.
Hayo yalisemwa na Ofisa mafunzo na mawasiliano wa idara ya kinga na chanjo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Ibrahim Maduhu wakati wa mkutano wa kamati ya huduma ya afya ya msingi wa jiji la Tanga.
Alisema kuwa uwekezaji huo ni mkubwa kufanywa na serikali kwa wananchi wake kwa lengo la kuwapatia afya bora.
Dk Maduhu alisema, kuwa ni jukumu la kamati za afya nchini nzima
kuhakikisha wanaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo.

“Ni vema mkahakikisha watu wanajitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo kwani limelenga kwa watoto kuanzia umri wa miezi tisa hadi miaka 15,” alisema
Naye mganga mkuu wa jiji hilo, Dk Asha Mahita alisema, kuwa asilimia 15 ya watoto waliopatiwa chanjo ya surua katika jiji hilo hawajajenga kinga kamili.
Alisema kuwa kampeni hiyo itawahusisha hata watoto waliopatiwa chanjo ya surua awali.
Alisema jiji hilo litakuwa na vituo 600 kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo kwa wananchi wote.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa