Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknorojia, January Makamba, ambaye ametangaza nia ya kugombea nafasi ya urais, amewaomba viongozi wa dini kuliombea Taifa ili uchaguzi mkuu ujao Watanzania wamchague rais mwenye hekima, busara na kutenda haki kwa wote.
Alitoa ombi hilo wakati akizungumzza na viongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga wakati wa jubilee ya kanisa la Mtakatifu Luka ya miaka 125 tangu kujengwa kwake wilayani Muheza.
“Tunawaomba viongozi wa dini waliombee Taifa kwa sababu hata wao pamoja na waumini wao wanapotaka kuchagua kiongozi wanaomba kwanza kabla ya kupiga kura wanamuomba Mungu awachagulie kiongozi bora, hivyo lazima utaratibu huo utumike kupata kiongozi mwenye busara, hekima na kutenda haki kwa watu wote kwa sababu uongozi wa nchi lazima apate Baraka za Mungu, alisema Makamba.
Katika sherehe hizo Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga, William Mahimbo Mndolwa, alisema kanisa lake litaendelea kushirikiana na serikali kwa huduma za kijamii.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment