Home » » JAMBAZI APIGWA RISASI NA WENZAKE

JAMBAZI APIGWA RISASI NA WENZAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MTU mmoja anayeshukiwa kuwa ni jambazi sugu, Benard Aaron (47) ‘Chinga’ amefariki dunia kwa kupigwa risasi na majambazi wenzake.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 8:00 usiku katika Kata ya
Majengo Wilaya ya Tanga, ambako majambazi wanne akiwemo mwanamke, walivamia nyumba ya mfanyabiashara Rashidi Mwacharo kwa dhumuni la kupora mali.

Mwacharo, aliiambia Tanzania Daima kuwa, majambazi hao walivamia nyumbani kwake na kuanza kurusha risasi alizozikwepa na ndipo ikampiga mwenzao na kumsababishia kifo.
“Walivyoona wamempiga mwenzao wakati mimi tayari nimelala chini na
majirani nao wakiwa wameamka, walimkokota na kutoka nae nje ili kukimbia,” alisema Mwacharo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Freisser Kashai, alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa, jambazi huyo alifariki dunia na wengine watatu walitorokea kusikojulikana na kwamba upelelezi unaendelea.
Kamanda Kashai, alisema majambazi hao walikuwa na silaha aina ya Pistol na
katika eneo la tukio kumeokotwa maganda mawili ya risasi huku mfanyabiashara huyo akijeruhiwa kichwani na mkono wa kulia, ambako amelazwa katika hospitali ya Bombo kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Hamisi Ramadhani, alisema alisikia kishindo kutoka kwenye mlango wa jirani yake na kutoka ili kujaribu kutoa msaada, lakini alishindwa kutokana na onyo lililotolewa na majambazi hao wakati wakijaribu kumsaidia  mwenzao aliyekuwa amepigwa risasi.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa