Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZAZI wametakiwa kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni ikiwa
ni pamoja na kushirikiana na walimu ili kuweza kuthibiti utoro.
Akizungumza juzi wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Haki na Ulinzi wa
Mtoto kwa klabu za wanafunzi shuleni kilichochapishwa na Shirika la
Passadit, Katibu Tawala Wilaya ya Tanga, Bernard Marselline, alisema
Mkoa huo unakabiliwa na tatizo la utoro hatua inayochangia kushuka kwa
kiwango cha elimu.
Marselline, alisema kuna aliwataka walimu kuhakikisha wanatoa taarifa
juu ya vitendo vya utoro na mimba shuleni na iwapo watashindwa kuripoti
matukio hayo hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa walimu hao.
Katibu huyo aliwakemea wazazi hao kuacha kuwaoza mabinti zao wakati
wakiwa shuleni na badala yake kusimamia kwa ukaribu maendeleo yao ili
wafanye vema katika masomo yao.
Naye Mratibu wa Shirika la Passadit, Simon Stephano, alisema shirika
lake kwa miaka mingi limekuwa likifanya utafiti mitaani na kubaini
ukatili wa kijinsia kwa watoto ukiendelea.
Alisema wamechapa kitabu hicho ili kuwawezesha jamii ya watoto kuelewa
haki zao hivyo kitabu hicho kitatoa muongozo hatua itakayosaidia
kutokomeza vitendo vya unyanyasaji vinavyofanyika katika jamii.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment