Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kwa Mwenyekiti
mpya wa Chama hicho wilayani Korogwe, Aulerian Nziku, amesema
wamejipanga kumng’oa Mbunge wa Korogwe vijijini, Stephen Ngonyani,
maarufu kama Profesa Majimarefu (CCM).
Akizungumza na Tanzania Daima juzi wilayani humo, Nziku ambaye ni
Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa alisema,
chama chake kitawahamasisha wananchi wa jimbo hilo ili kumg’oa Ngonyani
kupitia sanduku la kura kutokana na kushindwa kusimamia maendeleo.
Nziku alisema kuwa mbunge huyo amekuwa akiwakumbatia madiwani wazembe
ambao wameshindwa kuwatumikia wananchi ipasavyo na kuwa kero katika
jimbo hilo .
“Hatuwezi kuendelea kushuhudia wananchi wakikosanishwa na viongozi na
ndugu zao kwa imani za uganga badala ya kupelekewa maendeleo ya
kiuchumi jimboni,” alisema.
Hata hivyo Nziku alisema Korogwe vijijini wamekosa mtetezi kwani
fedha za mfuko wa jimbo hazifahamiki namna zinavyotumika, akitolea mfano
msaada wa fedha zilizotolewa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa, (UNDP) sh Mil. 253/-, ambazo hazieleweki zimefanya kazi gani.
Nziku alisema baadhi ya viongozi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi na kuwasababishia kuwa maskini.
Akizungumzia tuhuma hizo, Ngonyani alimtaka Nziku kwaweka wazi
madiwani ambao amewakumbatia kwani amejitaidi kuhakikisha miradi ya
maendeleo inatekelezwa kwa wakati
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment