Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MADUKA manne yameteketea kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme
barabara ya 14 jirani na stendi ya mabasi yaendayo mikoani jijini
Tanga, usiku wa kuamkia jana.
Moto huo uliozuka majira ya saa tatu na nusu usiku katika eneo hilo,
inaelezwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyosababishwa na
kutokuzimwa kwa baadhi ya vifaa.
Bakari Shabani ambaye ni shuhuda wa tukio hilo, alisema alishangaa
kuona moshi ukitoka juu ya mlango wa duka moja linalouza vifaa vya
umeme ndipo alipowaambia wenzake ili kutoa taarifa kwa Jeshi la
Zimamoto.
“Mimi nilikuwa katika biashara yangu ya chipsi jirani kabisa na
maduka haya, mara ghafla nikashangaa kuona moshi ukitokea kwa juu… si
ndipo nilipopiga kelele ili watu waje,” alisema Shabani.
Alisema kuwa Zimamoto walifika katika tukio na kuanza taratibu za
uokoaji ingawaje hawakufanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwani tayari vitu
vilivyokuwemo vilikuwa vimeshateketea.
Akizungumza na Tanzania Daima, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji Mkoa wa Tanga, Charo Mangare, alisema kuwa ni vema
wafanyabiashara kufunga mitungi ya kuzimia moto ‘Fire extinguisher’ ili
kutatua matatizo ambayo yanaweza kutokea katika majanga hayo ya moto.
Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki,
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na uchunguzi wa kubaini chanzo cha
moto huo unaendelea
Chanzo; Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment