Home » » KOROGWE WATEKELEZA AGIZO LA RAIS

KOROGWE WATEKELEZA AGIZO LA RAIS

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
MKUU wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Mrisho Gambo, amesema wilaya yake imetekeleza agizo la Rais la ujenzi wa maabara kwa asilimia 65.
Gambo aliyasema hayo hivi karibuni katika ya kutembelea ujenzi wa vyumba vya maabara unaoendelea katika kata mbalimbali wilayani hapa na kueleza kuwa wilaya hiyo ipo kwenye hatua nzuri ya makusanyo ya michango ya wananchi ambapo Novemba mwaka huu tatizo la maabara litakuwa limepatiwa ufumbuzi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya hiyo, Lucas Mweri, alisema mtendaji atakayeshindwa kusimamia kazi hiyo atakatwa mshahara wake, ili aone umuhimu wa na unyeti wa jambo hilo kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.
Diwani wa kata ya Mazinde, Abdalah Mangare, alisema wananchi wameona umuhimu wa ujenzi wa vyumba vya maabara na kukubali kuchangia.
  Chanzo Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa