Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BAADHI
ya wananchi wa Mji wa Mombo wamedai, hawajafurahishwa na Jeshi la
Polisi mjini hapa, kuzuia mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), na kuruhusu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanywa na
Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.
Kwa mujibu wa wananchi hao, walidai kuwa Polisi jana ilizuia kutoa
kibali kwa CHADEMA iliyoomba kufanya Mkutano katika Mji Mdogo wa Mombo
Ijumaa ijayo kisha kuruhusu CCM ifanye mkutano katika mji huo.
Polisi mmoja ambaye hakutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa jeshi
hilo, alikiri kuwa chadema wamenyimwa kibali kwa kuwa wameomba
maandamano na mkutano.
“CHADEMA walizuiwa kwa sababu waliomba Kibali cha Maandamano na
Mkutano, hivyo kwa kuwa maandamano yamepigwa Marufuku nchi yote,
hawakuruhusiwa kufanya hivyo na kwamba kitendo cha kufanya hivyo bila
kibali, watalazimika kuwatawanya.
“Ni kweli CCM wamekubaliwa kufanya Mkutano hapa Mombo Ijumaa,
Septemba 26, utakaohutubiwa na Kinana, na CHADEMA tuliwaruhusu kama
wanataka kufanya Mkutano wafanye Mombo, Septemba 26, lakini si
Maandamano”, alisema.
Mwenyekiti wa CHADEMA Korogwe, Aurelian Nziku, alisema kuwa waliomba
kibali cha kufanya maandamano ya amani na mkutano ila polisi imezuia
maandamano na kuruhusu mkutano wa CCM, ila wao pia wameruhusiwa kufanya
mkutano mwishoni mwa wiki.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment