Home » » WAKULIMA KUUZIWA HISA KAMPUNI YA KATANI

WAKULIMA KUUZIWA HISA KAMPUNI YA KATANI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kampuni ya Katani Ltd ya Mkoani Tanga, inatarajia kuuza asilimia 40 ya hisa ya kiwanda  usindikaji wa katani cha Mwelya kilichopo wilayani Korogwe kwa wakulima wadogo.
Akizungumza katika maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Sabasaba jijini Dare s Salaam jana, Meneja masoko wa kampuni hiyo, Shaidu Rajabu, alisema watakaonufaika na mpango huo ni wakulima 306 wa shamba hilo.

Rajabu alisema mpango wa kuwauzia kiwanda hicho upo katika hatua ya mwisho, ambapo wakulima hao watapata fursa ya kuwa wamiliki.

Hata hivyo baada ya kukamilika eneo hilo, zoezi hilo litaendelea kwa viwanda vilivyopo katika mashamba ya Hale, Magoma, Magunga  na Ngombezi.
“Tumeanza kwa wakulima wa shamba la Mwelya, nia yetu  ni kuwafanya wakulima wadogo kuwa sehemu ya wamiliki wa viwanda kwa ajili ya kuinua vipato vyao na uchumi wa Mkoa wa Tanga kwa ujumla,” alisema Rajabu.

Akizungumzia uinuaji wa zao hilo, Rajabu, alisema kampuni yake imesaidia kuinua kiwango cha uzalishaji kutoka tani 1,090 mwaka 2003 hadi kufikia tani 3,755 mwaka huu.

Aidha, kwa kutumia utaratibu wa (SISO) kampuni inawaendeleza wakulima wadogo kwa kusaidia kuwapatia pembejeo na zana ukuliza kilimo  kabla ya kuuziwa mazao kwa bei nzuri inayolingana na soko.

Rajabu, alisema kipato cha wakulima hao kimekua kwa kiasi kikubwa baada ya kilo moja ya katani aina ya Grade ug kutoka Sh. 1400 hadi Sh. 2000 ya sasa.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa