Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imeagiza kurejeshwa ardhi ambayo haiendelezwi na kuwapa
wananchi wanaokabiliwa na uhaba wa ardhi katika maeneo mengi hususani
mkoani Tanga.
Wito huo ulitolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akifunga
maadhimisho ya 10 ya Wiki ya Serikali za Mitaa yaliyofanyika kitaifa
katika viwanja vya Tangamano, jijini hapa.
Pinda alitoa agizo hilo kutokana na baadhi ya watu kuhodhi maeneo
makubwa ya ardhi mkoani hapa bila kuyaendeleza huku Watanzania wengine
wakiishi bila umiliki wa ardhi, hali inayosababisha ugumu wa maisha.
Alisema ni wakati wa kurejesha serikalini ardhi ambayo haiendelezwi
kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo badala ya kukaa bila shughuli
yeyote.
“Tunatambua serikali ina migogoro mingi ya ardhi, hivyo maeneo yote
ambayo hayaendelezwi tupewe orodha, ili apelekewe Rais Kikwete aweze
kuyatolea maamuzi na hatimaye wagaiwe Watanzania,” alisema Pinda.
Awali, Mwaenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT)
Taifa, Dk. Didas Masaburi, aliiiomba serikali kukubali kupitisha sera
ya kukuza uchumi katika ngazi ya halmashauri, kuongeza ajira kwa vijana
na wanawake sambamba na kukuza uchumi wa mtu mmojammoja pamoja na
kuingizwa kwa sura kamili ya serikali za mitaa katika mchakato wa
kupata katiba mpya.
Alisema ni vema sasa katika mchakato wa katiba mpya ikatambua uwepo
wa Serikali za Mitaa, kwani bila Serikali za Mitaa hakuna maendeleo
endelevu hususani katika suala zima la kuwaletea wananchi maendeleo
Chanzo;Tanzani Daima
0 comments:
Post a Comment