Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TANZANIA ni nchi ya tatu Afrika inayokabiliwa na tatizo la udumavu
wa watoto chini ya miaka mitano unaotokana na ukosefu wa lishe bora.
Hayo yalielezwa na Mkurungezi wa Taasisi ya Chakula na Lishe
Tanzania, Francis Mudaha alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa
ushawishi na utetezi wa uboreshaji masuala ya lishe mkoani hapa
uliojumuisha wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa wilaya na waganga wakuu
wa wilaya zote tisa za mkoa huu.
Alisema utafiti wa mwaka 2010 unaonyesha kwamba Tanzania unapoteza
watoto 1,600 kwa mwaka huku watoto watatu wanakufa kila mwezi kwa
utapiamlo.
Alisema hali hiyo inasababishia hasara ya zaidi ya sh milioni 815 ya
pato la taifa inayopotea kutokana na kuhudumia watoto wenye utapiamlo
maeneo mbalimbali nchini.
Mudaha alizitaja athari za utapiamlo kwa watoto kuwa ni kuathiri
ubongo, mifumo bora ya kinga za mwili na ukuaji dhaifu ikiwemo uwezo
wake wa kufikiri kwa haraka na kuchukua uamuzi.
Hata hivyo aliiomba serikali kuimarisha ulishaji wa watoto wachanga
ikiwemo kusisitiza umuhimu wa maziwa ya mama, kuhamasisha uzalishaji wa
vyakula mchanganyiko ili kuzuia utapiamlo kwa watoto chini ya miaka
mitano.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, alisema viwango vya utapiamlo
kwa watoto chini ya miaka mitano mkoani hapa ni asilimia 49.
Aliahidi kutoa ushirikiano katika kuhamasisha kipaumbele kwenye masuala ya lishe ili kupunguza ukubwa wa tatizo
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment