Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WIZARA ya Nishati na Madini imesema itahakikisha haitoi mwanya kwa
wawezezaji wababaishaji wanaotaka kuwekeza kwenye nishati ya umeme na
kuwaingiza Watanzania kwenye mgawo wa umeme bila sababu.
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakimu Maswi, alitoa kauli hiyo wakati
wa mkutano mkuu wa viongozi wa chama cha wafanyakazi, TUICO matawi ya
Shirika la Umeme (Tanesco) na viongozi wa wizara.
Alisema asilimia 24 ya Watanzania zaidi ya milion 44 ndio
waliounganishwa na huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali vijijini na
mijini.
Maswi alisema kiwango hicho kinaonyesha kwamba kuna watanzania wengi wanaotumia mkaa na kuharibu mazingira nchini.
Kwa sababu hiyo idadi serikali kupitia sekta ndogo ya nishati ya
umeme inadhaniria kuongeza idadi ya watumiaji wa umeme hadi kufikia
asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felichesmi Mramba, alisema
shirika hilo limeanza kufanya vizuri huku akisema ifikapo mwaka 2033
asilimia 75 ya Watanzania watanufaika na huduma hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, alisema mkoa huo
umedhamiria kuinua pato la mtu mmoja mmoja, hivyo anaamini kwamba
kupitia umeme Watanzania wengi watanufaika na huduma bora za shirika
hilo
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment