Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI inaandaa mpango wa kuomba wafadhili wa ndani na nje ya nchi
utakaowawezesha kujengea kiwanda cha kubangulia korosho kwa wakulima wa
zao hilo walayani Mkinga, Tanga.
Ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kumaliza tatizo la wakulima wa
korosho katika wilaya hiyo wanaouza zao hilo kwa walanguzi wa nchi za
jirani.
Akifungua semina ya siku tatu ya wakufunzi na wanafunzi wa mafunzo ya
korosho yaliyofanyika Maramba wilayani Mkinga, Mkuu wa Wilaya hiyo Mboni
Mgaza alisema uuzaji wa korosho kwa walanguzi ni changamoto kwa
wakulima.
Aliwaambia wadau wa semina hiyo iliyoandaliwa na Kituo cha Utafiti wa
korosho cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara kwamba kuvushwa kwa zao
hilo kwenda Kenya kunawafanya wakulima wapate bei ndogo kutoka kwa
walanguzi.
“Si hivyo tu athari nyingine ni upotevu wa mapato ya ushuru ambayo
yangepatikana iwapo korosho ingeuzwa katika soko rasmi na kuliingiza
pato taifa,” alisema Mgaza.
Mgaza alivitaka vijiji vya Mkinga leo, Mwanyumba, Horohoro na Kwangena
ambao ni wakulima wa korosho kuwa chachu ya kukataa kuuza zao hilo kwa
bei ndogo kwa walanguzi kitendo kinachodidimiza
vipato vyao.
vipato vyao.
Naye Dk. Louis Kasuga kutoka Chuo cha Utafiti cha Naliendele, alisema
mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha wadau kuboresha na kuyatunza
mashamba yao.
‘’Tunawahamasisha wapande mbegu bora zenye sifa zinazotakiwa ili
kupata mazao bora ya kutosha… wadau pia wafufue mikorosho
iliyotelekezwa,” alisema Dk. Kasuga.
Wilaya ya Mkinga inao wakulima 2,565 waliopo sasa tofauti na wakulima
1,089 waliokuwepo hadi mwishoni mwa mwaka jana, hali hiyo ni sawa na
ongezeko la wakulima 1,476.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment