Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
Kiwanda hicho kilifungwa na Serikali kufuatia mgogoro ulioibuka baina ya wakulima na Mwekezaji huyo, Shahdad Mullah.
Akizungumza na wakazi wa Mkoa wa Tanga, Waziri Mkuu , Mizengo Pinda alisema Serikali imeona suluhu ya mgogoro huo uliomudu kwa muda mrefu ni kukinunua kiwanda kisha kukiuza kwa mwekezaji mwingine.
“Kwa sisi huku ndani serikalini mgogoro umekwisha lakini lililojepesi kwa sasa ni serikali kuzungumza na mwekezaji ili akubali kutuuzia kile kiwanda…lengo ni kumnufaisha mkulima, ” alisisitiza Pinda.
Kuhusu mashamba yaliyotelekezwa na wawekezaji yaliyopo mkoani hapa, alimuagiza Mkuu wa mkoa na sekretarieti yake kuhakikisha wanaandaa orodha yake na kuiwasilisha kwake ili amshauri Rais Jakaya Kikwete yarudishwe kwa wananchi wenye lengo la kuwaendeleza.
“Hivi mtu yupo Uingereza shamba lipo Tanga akisikia tu wananchi wameanza kulima anaanza kulalamika eneo lake limevamiwa, sisi kama serikali hatuwezi kuivumilia hali hii na ni wakati mwafaka wa maeneo haya kurudi mikononi mwa wananchi wa eneo husika, ” alisema PindaKuhusu migogoro ya ardhi iliyopo wilayani Kilindi baina ya wakulima na wafugaji, alisema serikali imeanza kutafuta mbinu za kisayansi kutatua kufuatia baadhi kusababisha uvunjifu wa amani na vifo vya watu .
Kwa upande mwingine Pinda aliwaagiza mameya, wenyeviti wa halmashauri na madiwani kuwashirikisha wananchi kwenye shughuli za maendeleo miradi kwenye maeneo yao ili nao waweze kutoa vipaumbele kulingana na mahitaji halisi ya huduma wanayoitaka.
“Huku kutoshirikisha wananchi na kujidae wababe ndiyo kunakopelekea mwisho wa siku kwenye uchaguzi Diwani out pamoja na Mbunge wake kwani kazi waliyokutuma hufanyi …. wananchi ndiyo msingi wa serikali za mitaa na ustawi wa maendeleo, ” alisisitiza Pinda ambaye juzi alifungua sherehe za serikali za mitaa nchini ambazo kitaifa zinafanyika mkoani Tanga.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment