Home » » KESI YA MEJA WA JWTZ YAAHIRISHWA

KESI YA MEJA WA JWTZ YAAHIRISHWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
KESI ya shambulio iliyojeruhi na kusababisha upotevu wa zaidi ya sh milion 7.8 inayomkabili Ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Chuo cha Anga kilichopo Kange jijini Tanga, Meja Lemicho Msafiri, imeahirishwa.
Iliahirishwa mapema jana katika Mahakama Kuu Mkoa wa Tanga na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya, Ramla Shehagilo na kusema itaendelea Julai 28, mwaka huu.
Shambulio hilo lilifanyika dhidi ya mstaafu mwingine wa jeshi hilo ambaye kwa sasa ni balozi wa mtaa wa TRA/Jeshini, Nasibu Abdallah aliyevamiwa nyumbani kwake kisha kupigwa, kujeruhiwa na kuharibiwa thamani za nyumbani kwake Desemba 20, 2012.
Imeelezwa kuwa meja huyo alipewa taarifa kwa njia ya simu na mkewe akiwa nchini China kikazi na kujulishwa kwamba balozi huyo alikwenda
nyumbani kwake na kumtukana kitendo ambacho mlalamikaji amedai si kweli. Hata hivyo mshitakiwa huyo yupo nje kwa dhamana.
Chanzo;Tanzania Daima  

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa