Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Subila Mgalu
Alitoa ahadi hiyo jana wakati akizungumza na wananchi katika
mkutano wa hadhara uliyofanyika Kibaranga, baada ya kutokea mgogoro kati
ya wananchi na maafisa ardhi waliyopewa kazi ya kupima shamba hilo.
Alisema kuwa kazi ya kupima shamba hilo imeanza lakini kuna baadhi ya watu wanaendeleza mgogoro kati ya wananchi na serikali.
Hatua hiyo inafuatia maafisa ardhi wilaya ya Muheza kuanza kupima shamba hilo ili wananchi wapatiwe maeneo ya kilimo.
Alisema kuwa baadhi ya watu wanadanganya wananchi hao kuwa tayari
maafisa ardhi wanagawa mashamba kwa kupewa kitu kidogo, kitu ambacho si
cha kweli. Alisema amesikitishwa na kitendo cha wananchi hao kufukuza
maafisa ardhi kwa kutumia mapanga wakati mchakato huo ukiwa unaendelea
vizuri baada ya agizo la Rais Jakaya Kikwete la kukubali shamba hilo
wapewe wananchi.
Alisema kuwa kwa sasa wanafanyakazi hiyo ya upimaji kwa shida kwani
inatakiwa zaidi ya Sh. Milioni 100 lakini wanapima kwa Shilingi Milioni
nane tu ambazo wamepewa na wafadhili kufanya kazi hiyo.
Mgalu alisema kuwa yupo tayari kufa ili kuhakikisha shamba hilo linapimwa ili wananchi wapewe ardhi hiyo.
Aliwataka wananchi kuwa wavumilivu ili zoezi hilo liende vizuri ili wananchi wapate ardhi.
Kwa upande wake Afisa ardhi ambae alikuwa anaendesha zoezi la
upimaji shamba hilo, Daniel Mkwizu, alisema kuwa zoezi lilikuwa
linaendelea vizuri lakini wananchi waliwafukuza na mapanga na
kulisitisha.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment