Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu nane kwa tuhuma
za unyang’anyi wa sh 978,600 kwa kutumia silaha katika Kijiji cha
Jasini mpakani mwa Kenya na Tanzania.
Akithibitisha kutokea kwa uhalifu huo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Costantine Massawe, alisema ulitokea usiku wa kuamkia Juni 9, mwaka
huu.
Kamanda Massawe alisema watuhumiwa hao walimvamia mfanyabiashara,
Mohamed Tembo mkazi wa Jasini wakiwa na mapanga kisha kumpora pesa hizo
huku akibainisha watuhumiwa sita walikamatwa na wengine wawili
walitoroka.
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani hapa linawashikilia wakazi wawili wa maeneo tofauti kwa tuhuma za kupatikana na silaha kinyume na
sheria.
sheria.
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Jeofrey Daniel (20), mkazi wa Kwanjeka na Mussa Hamis (44), mkazi wa Mtambuwe.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, watuhumiwa hao walikutwa na silaha aina
ya Rifle yenye namba 2703520; risasi mbili, ganda la risasi, panga,
kisu, na bisibisi mbili na kueleza kuwa silaha hiyo ilikutwa maungoni
mwa Mussa Hamisi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment