Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kushirikiana na Kamati ya
Maudhui, imefanya ziara mkoani hapa ya kutembelea vituo vya habari kwa
lengo la kuangalia namna wanavyofanya shughuli zao.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Magreth Munyagi, alisema lengo la kutembelea vituo hivyo ni
kujua kanuni wanazotumia katika uendeshaji wa matangazo yao.
Munyagi alisema majukumu makubwa ya kamati hiyo ni kuhakikisha
wamiliki wa vituo hivyo wanasimamia kanuni na taratibu za uendeshaji wa
vituo vyao kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla na si vinginevyo.
“Tumeona ni vema tukafanya ziara hii ili tuzidi kuwaelimisha na
kuwakumbusha kanuni na taratibu tukiamini wengine mnakiuka kwa
kutokujua,” alisema Munyagi.
Naibu Mkurugenzi Idara ya Utangazaji wa TCRA, Fredrick Ntobi, alisema
wamiliki wa vyombo hivyo wanatakiwa kuhakikisha wanaboresha mazingira
ya wafanyakazi wao ikiwa ni pamoja na kusimamia ipasavyo mikataba yao.
“Wamiliki wa vituo wahakikishe wafanyakazi wanaowaajiri wanakuwa na
‘professional’ na weledi katika fani waliyoisomea, ili tasnia hii izidi
kukua siku hadi siku,” alisema Ntobi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment