Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
UONGOZI wa timu ya Coastal Union ya Tanga jana umefungua tawi la
wapenzi wa klabu hiyo liitwalo Dunia Hotel lililopo Kata ya Makorora
jijini hapa ikiwa ni harakati za kuimarisha umoja na mshikamano
miongoni mwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.
Akizungumza jijini hapa jana, Ofisa Habari wa timu hiyo,
Oscar Assenga, alisema, ufunguzi wa tawi hilo ni moja kati ya mikakati
ya timu hiyo kuhakikisha wanakuwa na wapenzi Mkoa mzima.
Assenga alisema, licha ya kufungua tawi hilo, bado
wanaendelea na harakati za usajili wa nguvu kwenye kikosi chao, lengo
likiwa ni kuwa na timu nzuri ambayo itatimiza ndoto zao za kushiriki
mashindano ya makubwa yakiwemo ya Kombe la Shirikisho (CAF), siku
zijazo.
Alisema, bado wanaendelea kucheza mechi mbalimbali za
kirafiki, ili kuimarisha kikosi chao cha U-20, ambacho kitashiriki
mashindano mbalimbali yakiwemo ya Kombe la Uhai na Rolling Stone.
Katika hatua nyingine, Assenga alisema, kikosi cha timu ya
pili kinatarajiwa kufanya ziara ya kimichezo kwenye Wilaya mbalimbali,
lengo likiwa kuwapa burudani wakazi wa Mkoa huu.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment