Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMPUNI ya Katani ipo kwenye hatua za mwisho za mazungumzo kuhusu
ukubwa wa kiwanda cha kuzalisha sukari kutokana na mabaki ya mkonge,
itakayotumika kwa wagonjwa wenye kisukari.
Hayo yamesemwa na Mkurungezi wa Maendeleo Katani Juma Shamte
alipozungumza kwenye semina ya wazi iliyofanyika kwenye viwanja vya
Tangamano jinsi wakulima watavyonufaika na mkonge.
Alisema kuwa kwasasa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na kampuni
itakayojenga kiwanda hicho nchini kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa
bidhaa hiyo hapa nchini.
Shamte alisema kiwanda hicho kitakapo kamilika ujenzi wake na kuanza
kazi kitawezesha kupungua uhaba wa sukari nchini na nyingine kuuzwa
kwenye masoko ya kimataifa.
Kwa upande wa mahitaji kwenye soko la dunia, Shamte alisema uhitaji
wa bidhaa za mkonge umezidi kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 15 ya bei
ukilinganisha na mwaka 2000 ambapo bei ilikuwa chini.
Hata hivyo aliwahimiza wakulima kulima mkonge kwa wingi ili
kujiongeza kipato maradufu kutoka na zao hilo kuwa na soko la uhakika
ndani ya nchi na hata nje ya nchi.
"Mfumo wa masoko si wa kugawana mapato kwani zao hili linamuwezasha
mkulima kupata mapato yake mwenyewe na kampuni ya katani kazi yake ni
kumuwezesha mkulima kupata pembejeo pamoja na kumtafutia soko la
uhakika la kuuza bidhaa zake,"alisema Shamte.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment