Marehemu Lt. Col. Mstaafu Maurice Noel Singano enzi ya uhai wake.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ
Kikosi cha 37, likiwasili katika makaburi ya Bombo mjini Tanga kwaajili ya
mazishi.
Shughuli za mazishi
zikiendelea.
Shughuli za uwekaji wa
mashada ya maua zikiendelea.
Askari wa JWTZ 37KJ
wakifanya mazishi ya kijeshi, ikiwa ni pamoja na kupiga risasi kadhaa hewani.
Mwili
wa Marehemu Luteni Kanali mstaafu, Maurice Noel Singano ukiwasili
nyumbani kwa mtoto wake Mikocheni B jijini Dar es Salaam Alhamisi Juni
05.2014, kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Tanga kwa mazishi
yaliyofanyika Ijumaa Juni 06.2014. Marehemu Mzee Singano alifariki Mei
31, mwaka huu huko katika Hospitali ya Appolo Chennai nchini India
alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata mshtuko.
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akiwa na wafiwa alipokwenda kuhani msiba Mikocheni B jijini Dar.
Waziri
Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim akitoa heshima za mwisho kwa mwili
wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. John Haule
akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga
Mikocheni B jijini Dar.
Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha siasa cha Democratic Party (DP), Mchungaji
Christopher Mtikila akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu
wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
) Dada za Marehemu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga Mikocheni B jijini Dar.
Jeneza
lenye mwili wa marehemu likiingizwa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu
Martha lililopo Mikocheni B jijini Dar, kwaajili ya misa kabla ya
kuanza safari ya kuelekea Tanga kwa mazishi.
Maafisa
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 37 Tanga, wakitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu wakati wa kuuaga nyumbani
marehemu katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Mjane wa Marehemu, Bi. Maria Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa mpendwa mume wake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Mtoto
wa Marehemu, ambaye ni Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel, Bi. Beatrice Singano akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili
wa mpendwa baba yake, nyumbani kwao katika eneo la Sahare mkoani Tanga.
Jeneza
lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha
37, likitolewa nyumbani katika eneo la Sahare mkoani Tanga kwaajili ya
kwenda kanisani na baadaye mazishi katika makaburi ya Bombo mkoani humo.
Aliyeshika Msalana ni mototo wa Marehemu, Bw. Billy.
Jeneza
lenye mwili wa Marehemu, likiwa lemebebwa na askari wa JWTZ Kikosi cha
37, likiwasili katika Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga
kwaajili ya misa kabla ya mazishi.
Padri wa Kanisa Katoliki la Mt. Mathias mjini Tanga akifanya sala kwa marehemu.
Wombolezaji kanisani
0 comments:
Post a Comment