Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MWENYEKITI wa Kamati ya Shule ya Msingi Amboni iliyopo nje kidogo
ya Jiji la Tanga, Amiri Mlugu, amepiga marufuku wanafunzi wa shule hiyo
kwenda katika majumba ya starehe ikiwemo vibanda vya kuonyeshea video
vilivyopo mitaani.
Mwenyekiti huyo ameeleza hayo katika kikao cha wazazi, wanafunzi na
walimu kilichofanyika shuleni hapo jana kwa ajili ya kupanga mikakati
ya kuleta ufaulu mzuri kwa wanafunzi wa darasa la saba kwenye mitihani
yao ijayo.
Malugu pia aliwataka wazazi na walimu kushiriki katika utekelezaji wa
agizo hilo ambalo litasaidia kuwakabili wanafunzi wenye tabia kama
hizo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment