SHIRIKA la Atomtek Nuclear Energy Track limeahidi kujenga zahanati katika Kijiji cha Kitumbi, Kata ya Mkata, Handeni, Tanga.
Kwa sababu hiyo ujenzi wa zahanati hiyo utawanufaisha wakazi wa Mkata
na viunga vyake ambao katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru wa
Tanganyika haijawahi kupata zahanati na kusababisha wajawazito kupoteza
maisha wakati wa kujifungua.
Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Mwenyekiti wa kijiji
hicho, Athuman Abdallah, alilishukuru shirika hilo kwa kukubali
kuwajengea zahanati hiyo huku akisema itapunguza vifo vya wajawazito na
watoto.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment